Header Ads


CHADEMA WACHANGIA MIFUKO 60 YA SARUJI UJENZI WA ZAHANATI

Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Chama cha Demkorasia na Maendeleo Mkoa wa Njombe Wamechangia Mifuko 60 ya Saruji Yenye Thamani ya Shilingi Laki 620 Kwa Ajili ya Ujenzi wa Zahanati ya Mtaa wa  Kihesa Ili Kuwasaidia Wananchi Hao Kuondokana na Adha ya Kufuata Huduza Za Afya Umbali Mrefu.


Image result for CHADEMAUjenzi wa Zahanati Hiyo Ambao Unatarajia Kuanza Mapema Baada ya Kukamilia Kwa Baadhi ya Taratibu Kutoka Kwa Mhandisi wa Halmashauri ya Mji Njombe Ambao Unatarajia Kugharimu Kiasi cha Shilingi Milioni 24 Kwa Awamu ya Kwanza ya Ujenzi wa Msingi.

Akizungumza Wakati wa Kutoa Mifuko Hiyo Diwani Viti Maalumu Kupitia chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Jimbo la Njombe Mjini Siglada Mligo  Amesema Kuwa Mwamko wa Wananchi na Viongozi wa Mtaa wa Kihesea Ndio Umewasababisha Kuchangia Michango Hiyo Ili Kutoa Hamasa Kwa Wananchi Wengine.

Nikson Kilasi ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Kihesa Ambaye Amesema Mwamko wa Wananchi Ambao Umeonekana Katika Ujenzi wa Miradi Mbalimbali Mtaani Hapo Kama Maji na Vyumba vya Madarasa Ndio Umewapa Hamasa ya Kuanza Ujenzi wa Zahahanati ya Mtaa Huo Pamoja na Kuwashukuru Viongozi Hao Kwa Kujitoa Kwao.

Nao Baadhi ya Wananchi wa Mtaa Huo Wamesema Kuwa Mtaa wa Kihesea Una Wakazi Zaidi ya Mia Nane Lakini Hauna Zahanati na Kupitia Umoja Walio Nao Kwa Makubaliano Wameridhia Kwa Nia Moja Ujenzi Huo  Ambapo Pia Wamewaomba Wadu Mbalimbali Kusaidia Kuchangia Ili Zahanati Ikamilike Kwa Wakati.

viongozi Hao Walio Changia Mifuko Hiyo ya Saruji ni Pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu CHADEMA Mkoa wa Njombe Lucia Mlowe Aliyetoa Mifuko 40,Diwani Viti Maalumu Siglada Mligo Mifuko 10 na Jeni Mgeni Katibu wa Baraza la Vijana Chadema Bavicha Ambae Naye Amechangia Mifuko Kumi Kwa Ajili ya Kuchangia Ujenzi wa Zahanati Hiyo ya Mtaa wa Kihesa

No comments

Powered by Blogger.