Header Ads


LIL KIM NA TUHUMA ZA UJAMBAZI

Rapa wa kike Lil Kim anachunguzwa na polisi mjini Los Angeles baada ya kuhusishwa na ujambazi uliotokea usiku June 25.

Image result for Lil Kim

TMZ imeripoti kuwa Lil Kim na kundi lake waligombana na mwenye nyumba aliyewakodishia eneo la kukaa wakati wanahudhuria tuzo za BET na ugomvi huu ulitokea baada ya Lil Kim kukata kulala eneo hilo sababu hakulipenda na kudai arudishiwe pesa yake.

Polisi waliitwa ila hawakuweza kufanya chochote kwenye ugomvi huo na baadae saa 10 usiku walirudi majambazi wakiwa na silaha na kuiba kitabu cha cheki cha Lil Kim na dola $20,000, ‘Milioni 40 za Tz’.

Kim alikuwa kwenye tuzo za BET Kwaajili ya show ya kutoa heshima kwa msanii wa kundi la Mobb Deep aliyefariki dunia June 20 Prodigy,42

No comments

Powered by Blogger.