Header Ads


Migos walivyopigana na kundi la vijana wa Chris Brown kwenye tuzo za BET

Stori kubwa kwenye Back Stage ya tuzo za BET ilikuwa beef kati ya kundi la wasanii wa rap la Migos na washkaji wa msanii wa rnb Chris Brown.

“Shuhuda anasema Chris alikuwa akipiga stori na washkaji zake ila baada ya kuona wasanii wa Migos wanakuja alinyamaza na kuanza kuondoka eneo hilo ila rafiki wa Chris Brown alimsukuma msanii wa Migos ‘Quavo’ na hapo ndio ngumi zikaanza kurushwa”

Taarifa zinasema kutokana na matatizo ya kisheria anayokabiliana nayo Chris Brown, hakuweza kukaa eneo hilo na kuamua kuondoka wakati ugomvi unaendelea.

Ugomvi wa Migos na Chris Brown ni kutkana na msanii wao Quavo kuwa na mahusiano na Ex wa Chris Brown ‘Karrueche Tran’

Huu sio ugomvi mmoja tu Migos wamekutana nao wiki hii, baada tu ya tuzo Migos walikuwa kwenye interview na DJ Akademiks  na imetajwa kuwa waligombana na rapa Joe Budden kwenye Mahojiano Hayo

No comments

Powered by Blogger.