Header Ads


OPARESHENI YA KUWAONDOA MACHINGA KATIKA KITUO CHA MABASI NJOME

Umoja wa wafanyakazi katika Kituo  Kikuu Cha mabasi mkoani njombe umeazimia kuwaondoa wafanyabiashara wadogo  maarufu Kama MACHINGA wanaofanya kazi ndani ya Kituo Hicho  kwa madai kuwa wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya wizi pamoja na kutozingatia kanuni za usafi wa mazingira.
Image result for MACHINGA NJOMBE
Mwenyekiti wa stendi kuu ya mkoa wa njombe Bwana Laito mwaipopo baada ya mkutano wa wafanyakazi uliokuwa na maazimio mbalimbali amesema kuondolewa kwa machinga Hao kutafanyika sanjari na kuwazuia wafanyakazi wa kike katika stendi.

Kamati ya ulinzi ya stendi iliyoteuliwa  imesema kumekuwa na utaratibu holela katika utoaji huduma kwa abiria ikiwemo vitendo vya uzalilishaji kwa abiria wa kike.

Kwa upande wao machinga wanaofanya kazi katika stendi hiyo wamesema kitendo cha kutaka kuwaondoa   ni hatua ya kuenaendelea kupigwa vita kila upande kuanzia halmashauri ya mji njombe  na uongozi wa stendi.

No comments

Powered by Blogger.