RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI, ALLY HASSAN MWINYI ASHIRIKI NA WATOTO YATIMA KATIKA FUTARI ILIYOANDALIWA NA AAR INSURANCE
Rais
Mstaafu awamu ya pili Mhe. Ally Hassan Mwinyi (Kushoto) akimpa
maelekezo ya chakua alichokuwa anakula wakati aliposhiriki hafla fupi ya
kufuturisha watoto Yatima wa kituo cha Kigogo iliyoandaliwa na Kampuni
ya Bima ya AAR jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa wakipakua futari.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Bima ya AAR wakiwapakulia wageni futari.
Mwenyekiti wa Bodi wa kampuni ya Bima ya AAR, Agnes Batengas akiwangoza watoto kwenda kuchukua futari.
Rais Mstaafu wa Awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi akitoa machache mara baada ya kukaribishwa kutoa nasafa zake.
Mwenyekiti
wa Bodi wa kampuni ya Bima ya AAR, Agnes Batengas akitoa shukrani zake
za pekee kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi mara
baada ya kushiriki futari na watoto yatima wa kituo cha kigogo jijini
Dar es Salaam.
Meneja
Masoko na Mauzo Kampuni ya AAR Insurance Tabia Masoud akiwahudumia
chakula watoto Yatima kutoka kituo cha Kigogo katika hafla fupi ya
kufuturisha iliyofanyika jijini Dar es salaam.
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi akitoa shukrani zake za
pekee mara baada ya kushiriki futari na watoto yatima wa kituo cha
kigogo iliyoandaliwa na kampuni ya Bima ya AAR.
Mkurugenzi
Mkuu wa kampuni ya Bima ya AAR, Violeth Mordichai akizungumza wakati wa
hafla fupi ya kufuturisha watoto Yatima kutoka kituo cha Kigogo jijini
Dar es salaam.
Rais
Mstaafu awamu ya pili Mhe. Ally Hassan Mwinyi (Kulia) akimkabidhi wa
zawadi na Mwenyekiti wa Bodi wa kampuni ya Bima ya AAR, Agnes Batengas
(Kushoto) wakati wa hafla fupi ya kufuturisha watoto yatima kutoka
kituo cha Kigogo jijini Dar es salaam jana.
Wafanyakazi
wa Kampuni ya Bima ya AAR wakipiga picha ya pamoja na watoto Yatima
mara baada ya kuwakabidhi zawadi katika hafla fupi ya kufuturisha watoto
yatima kituo cha kigogo jijini Dar es salaam na kuwapa misaada ya
chakula, nguo na viatu kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Fitri.
---
Dar
es salaam: Kampuni ya Bima ya AAR imefuturisha watoto yatima kutoka
kituo cha kigogo Jijini Dar es salaam. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na
Raisi Mstaafu awamu ya pili Mhe. Ally Hassan Mwinyi, pamoja
nawahamasishaji mbali mbali katika jamii wanaigusa jamii kwa namna
tofauti tofauti.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo Raisi Mstaafu hawamu ya pili Mhe. Ally Hassan
Mwinyi alishukuru kampuni hiyo kwa hafla hiyo ya pamoja kwa kuweza
kufuturu na watoto yatima na kugawa mahitaji mbalimbali ikiwemo nguo,
viatu na vyakula.
“Ningependa
kuwashukuru kampuni ya AAR kwa futari hii pia kuwapongeza katika kazi
mbali mbali mnazofanya katika kusaidia jamii kwa ujumla uhusani kwenye
swala la afya. Mwezi huu unatukumbusha kufanya yaliyo mema, kusaidia
wasiojiweza, kusamehana na kukumbushana mda wa ibada.” Alisema
Aidha
wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Violeth Mordichai
aliwakabidhi watoto hao mahitaji hayo na kuongeza kuwa, futari hiyo ni
sehemu ya mpango wake kusaidia jamii hivyo ni vyema katika kipindi hiki
wakafuturu pamoja na watoto hao.
“
sisi kama kampuni ya Bima iliyojikita katika kusaidia jamii kwenye
swala la afya tumeona ni jambo jema katika kipindi hiki cha mfungo wa
Ramadhani tukapata chakula cha pamoja na watoto yatima kutoka kituo cha
kigogo na kuweza kusaidia kwa kuwapa msaada wa mahitaji madogo
yatakayoweza kuwasaidia ,hata kipindi cha sikukuu ya Eid el fitri ”
alisema
Pia
aliongeza na kusema kwa wale ambao hawajajiunga na huduma zinazotolewa
na Kampuni hio wajiunge ili kupata huduma bora ya afya.
No comments