Header Ads


RIHANNA AMPA SHABIKI YAKE WAKIUME ALICHOKITAKAMuigizaji na Staa wa muziki wa RnB anayezidi kuwaka zaidi kupitia kazi ya ‘Wild Thoughts’ akiwa na Bryson Tiller waliyoshirikishwa na Dj Khaled, Rihanna amempoza maumivu kwa ushauri kuhusu mahaba shabiki aliyetaka kujua.

Picha linaanza kupitia mtandao wa Twitter wa shabiki anayetumia jina @WaladShami kwa kuamuandikia Rihanna kwa swali la kuwa ni kwa namna gani aliweza kuondokana na maumivu mara ya kwanza ya kutendwa? Na kuongeza kuwa ‘Nimekuwa nikijitahidi’ Swali ambalo Rihanna hakulikalia kimya.

Walad Shami

Ujumbe wa swali hilo Rihanna alimuandikia ‘Amini tu kuwa kutendwa ni zawadi yenyewe! Lia pale unaposhindwa, lakini haitakuwa milele! Utapata pendo tena na litakuwa zuri zaidi! kwa sasa unaweza kufurahia’ lilikuwa jibu kupitia ujumbe wa moja kwa moja kwa mujibu wa Screenshot ya maongezi. 

No comments

Powered by Blogger.