Header Ads


RPC NJOMBE:-WASIWEPO WA KUWATISHA WATAALAMU WA TIBA MBADALA

Image result for polisi tanzania

Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Limepiga Marufuku Tabia Za Baadhi ya Watu Kuendelea Kuwatisha Wataalamu wa Tiba za Asili na Tiba Mbadala Ambao Wamekuwa Wakifanyakazi Kubwa ya Kuokoa Maisha Ya Watanzania.

Kauli Hiyo Imetolewa na Mkuu wa Kituo Cha Polisi Uwemba Betinego Mwangasa Kwa Niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa Akiwa Katika Hafla ya Tathmini ya Muenendo wa Kituo Cha Matola Private Hospital Kinachomilikiwa na Tabibu Hussein Abdul  Ally Maarufu Kwa Jina la Fundi Sui Baada ya Kugundulika Kuwepo Kwa Baadhi ya Watu Wanaofika na Kumfanyia Vitisho.

Taarifa ya Kituo Hicho Iliyosomwa na Mwenyekiti wa Baraza la Kituo Bwana Ignas Mligo Imeeleza Kuwa Hadi Sasa Kituo Hicho Kimefanikiwa Kupokea Wagonjwa Zaidi ya 4000 Toka Katika Hospitali Mbalimbali Hapa Nchini na Kuwatibu Ikiwa Kati Yao ni Vifo Vinne Pekee Vilivyotokea.

Awali Baadhi ya Watu Waliopatiwa Huduma ya Matibabu na Wanaoendelea Kuhudumiwa Katika Kituo Hicho Wamekiri Kuokolewa Maisha Yao Kupitia Kituo Hicho.

Kwa Upande Wake Tabibu Hussein Fundi Sui Amesema Hadi Sasa Amepata Hasara ya Zaidi ya Shilingi Milioni Tatu Kutokana na Maswahibu Ambayo Amekuwa Akiyapata.

No comments

Powered by Blogger.