Header Ads


WANACCM NJOMBE WATAKIWA KUJIEPUSHA NA MAKUNDI KUELEKEA UCHAGUZI


Image result for chama cha mapinduzi ccm
Wanachama wa chama cha mapinduzi mkoani Njombe wametakiwa kujiepusha na makundi kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani ya chama hicho ili kuepusha kuibuka kwa migogoro baina yao kitendo ambacho kimedaiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kudhohofika kwa vyama vya siasa hapa nchini.

Rai hiyo imetolewa na katibu wa wawazi CCM mkoa wa Njombe Bw  Lukas Nyanda  wakati akiongea na UPLANDS FM Ofisini Kwake ambapo amesema chama hicho hakihitaji kuibuka kwa migogoro kwa mara nyingine kama ilivyokuwa 2015 hivyo yeyote atakaebainika kufanya hivyo atashughulikiwa haraka iwezekanavyo ili kuimarisha imani na umoja kwa wanachama wake.

Kuhusu masuala ya rushwa katibu huyo amesema chama kimejiimarisha vyema kufuatilia nyendo za wagombea na wanachama na kwamba kwa kuwa kila mmoja anatambua madhara ya rushwa CCM mpya imedhamilia kutokomeza vitendo hivyo.

Kwa upande wao wanachama wa CCM mkoani hapa akiwemo Daiel Richard Mhanja katibu umoja wa vijana wilaya ya Njombe wanasema wameridhishwa na mchakato unavyoendelea kwani umekuwa wa haki na uwazi lengo likiwa ni kuwapata viongozi ambao wataendana na kasi mwenyekiti wa chama taifa Dr.Magufuli huku wakidai wamejipanga vyema kukabiliana na wanachama mamruki kutoka vyama pinzani.

Wakati fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi zikiwa zinatarajiwa kuanza kutolewa bure hapo july 2 na kuhitimishwa july 10 katibu huyo wa wazazi mkoa wa Njombe Bw Nyanda anasema kutokana na utendaji na uwajibikaji mzuri wa Katibu wa wazazi taifa Bw Abdalah  Bulembo jumuiya hiyo imependekeza tena kiongozi huyo kugombea nafasi hiyo.

No comments

Powered by Blogger.