Header Ads


Drake awekeza kwenye biashara ya migahawa ya chai na kahawa

Rapa Drake ametajwa kuwa mwekezaji mpya kwenye biashara ya migahawa ya chai na kahawa ya New York #MatchaBar.

Kwa sasa kampuni hii inatangaza vinywaji vyao kama vinywaji vya Energy kama Kahawa au RedBull huku kauli mbiu yao ya biashara ikiwa ni ‘Better Energy’.

Kampuni hii ilianza kama mgahawa wa Kahawa huko Williamsburg mwaka 2014 na sasa wapo mpaka mjini  LA.

Baada ya uwekezaji wa Drake sasa kinywaji hichi kitapatikana kwenye chupa na kusambazwa kwenye miji mingi zaidi Marekani kwa kutumia umaarufu wa Drake.

No comments

Powered by Blogger.