Header Ads


Hongera Hamisa Mobeto kwa kujifungua ‘king’

Gulu wa mitindo Hamisa Mobeto leo amejifungua mtoto wa kiume, kupitia akaunti yake ya instagram amejipongeza na kumshukuru Mungu kwa kujifungua salama.

Hamisa bado hajaweka wazi kuhusu mzazi mwenza wa mtoto aliyezaliwa leo.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa mwanadada huyo kuingia leba, mara ya kwanza alijifungua mtoto wa kike ambaye mzazi mwenza anajulikana kwa jina la Majizzo ambapo mahusiano ya wawili hao yalivunjika na kumfanya kila mmoja kwenda na njia yake.

Kipindi gulu wa mitindo huyo, Hamisa Mabeto akiwa amebeba mimba amekuwa akipenda sana kupost picha ya ujauzito na kuweka maeno yaliyoleta utata mwingi mitandaoni na kupelekea mashabiki wake kumhisi baba mzazi wa kiumbe kilichozaliwa leo.

Kupitia kurasa za Insatagram za Hamisa Mobeto amekuwa akiandika maneno kama ”Mama Dee”, yaliyoleta tafsiri ya kuwa Diamond ndiye mzazi mwenza. Japokuwa Hamisa bado hajaliweka hilo wazi.

Mmoja ya marais wa wambea Tanzania, Soudy Brown ametumia ukarasa wake wa instagram kumpa hongera za dhati Hamisa Mobeto,”Hongera Bwana N na Bi H kwa kupata Dume la Mbegu” ameandika Soudy Brown, ambapo watu wameandika maoni yao na kumaanisha kuwa H inasimama kwa bi Hamisa huku N ikisimama kama kiashiria cha herufi ya mwanzo ya Naseeb yaani Diamond.


No comments

Powered by Blogger.