Header Ads


MRISHO NGASA KUTUA JANGWANI

Klabu ya soka ya yanga inatarajiwa kumtangaza nyota wake wa zamani mwisho Khalfani Ngasa kuwa mchezaji wao kwa Mara nyingine kabla ya dirisha la  usajili kufungwa usiku wa Leo.
Nyota huyo ambaye msimu uliopita alikua akiichezea Mbeya City anatajwa kuwa katika mazungumzo ya mwisho na uongozi wa mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara..

Ngasa ambaye amefanikiwa kuvichezea vilabu vya Simba na Azam hapa nchini kwa nyakati tofauti anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na wanajangwani hao.

Taarifa za ndani kutoka klabuni hapo zimearifu kuwa tayari winga huyo ameshamalizana na kamati ya usajili iliyo chini ya Mwenyekiti Hussein Nyika.

Ikumbukwe Ngasa aliondoka Yanga na kusajiliwa katika klabu ya Free State ya nchini Afrika Kusini lakini hakudumu na kikosi hicho  baada ya kuamua kuondoka kwa makubaliano ya pande zote mbili na baadae nyota huyo alijiunga na Fanja FC ya Oman ambako  pia hakupata nafasi ya kucheza kutokana na kuandamwa na majeruhi.

Aliamua kurejea nchini na kujiunga na mbeya city katika dirisha Dogo lA usajili ingawa baadae alitajwa kutaka kurejea yanga lakini ikashindikana.

Ngasa ambaye alishawahi kuichezea vilabu vya Toto Africans na Kagera Sugar anatajwa kuziba pengo  la Simon Msuva aliyetimkia nchini Morocco kucheza soka la  kulipwa..

No comments

Powered by Blogger.