Header Ads


MSIGWA ASEMA CHAMA CHA MAPINDUZI KIMECHOKA


Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kulitaka jeshi la polisi nchini kutokisaidia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema wamuache yeye na CHADEMA wapambane kukiondoa chama hicho madarakani kwani kimeshachoka

Msigwa amesema kitendo cha polisi juzi kumkamata wakati akiwa kwenye majukumu yake ya kibunge kimemuudhi sana na kusema ni jukumu la Mbunge yoyote yule kuelimisha jamii, kuwapa habari wananchi pamoja na kuikosoa serikali.

"Mimi nilikuwa sifanyi uchochezi kazi ya Mbunge kuelimisha, kuhabarisha, kuikosoa, kuisimamia serikali na kuchochea maendeleo katika jimbo kwa hiyo kama Mbunge ninayo haki ya kuzungumzia Demokrasia na haki ya kuzungumzia mambo ya utawala bora, nina haki ya kuzungumzia haki za binadamu , kitendo cha polisi kunikamata juzi kimeniudhi sana hao polisi waniache mimi na chama changu tupambane na CCM, wasiisadie CCM kwani saizi imechoka ipo dhohofu yaani ipo taabani wanajaribu kuitetea CCM, wajitokeze CCM wenyewe wajibu hoja" alisema Msigwa

Msigwa aliendelea kusema kuwa yeye ni Mbunge ana haki ya kuikosoa serikali iliyopo madarakani hata kuichonganisha na wananchi ili wasiichangue tena mwaka 2020 anadai huo ndiyo wajibu wake kisiasa na ndiyo maana anakuwa mpinzani

No comments

Powered by Blogger.