Header Ads


TANGA: WATU WAWILI WAKUTWA WAMEFARIKI GEST.

Watu wawili wamekutwa wamefariki katika nyumba ya kulala kwa wageni iliyojulikana kama Bomai Inn iliyopo Mabanda ya Papa Kata ya Majengo mjini Tanga,


Akidhibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amesema kuwa asubuhi wakati mfanya usafi anaingia aligundua uwepo wa miili hiyo.
“Asubuhi wakati anaingia kufanya usafi aligundu akuwepo kwa miili ya watu wawili ambao walikutwa wamekufa katika chumba namba 303 watu hawa kwa kifupi hawaja fahamika majina yao wote ni wanaume,” alisema Kamanda Wakulyamba.
“Wanakadiliwa kuwa na umri kati ya miaka 35 na 45 ingawa kwa mujibu wa taarifa ya mlinzi wa nyumba hiyo ya kulala wageni anadai kwamba mmoja kati ya marehemu hao alijitambulisha kwa jina Rahid Omary, kabila lake ni Msafwa na ni mfanya biashara na alijitambulisha kuwa anatokea jijini Dar es salaam.”

No comments

Powered by Blogger.