Header Ads


VIDEO VIXEN NA MSANII AMBER LULU AWACHANA WASANII WENZAKEWimbi la video vixen kuhamia katika kuimba limeonekana kukuwa kila kukicha. Amber Lulu amewachana wasanii ambao wamekuwa wakiwachukia warembo hao wa video wanapoamua kuingia katika tasnia ya kuimba.

Kazi ya video vixen Bongo imekuwa ikichukuliwa isiyofaa na haieleweki huku warembo wake wakionekana wenye tabia mbaya kupita kiasi. Akiongea na Bongo5, Lulu amesema, “Kitu kibaya walikiona kwao, kwa sababu kila siku wapo na unavyozidi kuwepo kila siku kila msanii unatakiwa kuwa na kitu kipya.
“Wao waavyoona watu wapya wanavyozidi kutokeza katika kitu wanachokifanya wao hizo ni jelous tu. Nadhani kitu kizuri wao wanatakiwa kufanya ni kutupa support sisi halafu kuona mwisho wa siku utakuwaje,” ameongeza.
“Wao wanang’ang’ania hili game hawataki watu wapya halafu hawataki watu wapya wakati wao hawana vitu vipya vya kufanya watu kuwavutia. Sisi ndio watu tunavitu vipya watu wanataka kuangalia mambo mengine kabisa sio kila siku unamuona nani kasimama kwenye steji na MIC yake anaimba tu.”
No comments

Powered by Blogger.