Header Ads


Baada ya G Nako kufanya cover ya Seduce Me, ‘mambo ya team yakae mbali’

Msanii wa kundi la Weusi, G Nako ameelezea mafanikio ya cover ya ngoma Seduce Me ya Alikiba aliyofanya.G Nako ambaye kwa sasa anatamba na ngoma ‘Energy’ amekiambia kipindi cha Clouds E kuwa mapokezi ya ngoma hiyo yamekuwa makubwa lakini mambo ya u-team katika muziki hayataki.
“Kwanza kabisa sitaki masuala ya ma-team, kuna vitu kidogo yanakuwa yanatuwekea mipaka, mambo ya team yakae mbali halafu muziki mzuri ndio uongee lakini so far mapokezi ni makubwa” amesema G Nako.
G Nako anaungana na producer Man Water na wasanii wengine mbali mbali ambao wamefanya cover ya ngoma hiyo.

No comments

Powered by Blogger.