Header Ads


INAWEZEKANA HUU NI UJUIO MPYA WA BELLAMuimbaji huyo akizungumza na Uplands fm kwenye xtra flava  amesema si kweli amefunga ndoa kama inavyozungumzwa na picha kuonekana ila itakafika wakati atazungumza.

“Kwa sasa hivi nitadanganya siwezi kuzungumzia hilo suala, kuna wakati nitazungumzia tu ila kuna vitu fulani naviweka sawa. Hapana siwezi kusema nimefunga ndoa au sijafunga ndoa” amesema Enock Bella.

Hapo jana wasanii wenzake aliokuwa nao Yamoto Band, yaani Aslay, Beka Flavor na Maromboso walionekana kumpongeza Bella kupitia mitandao ya kijamii kwa kuashiria amefunga ndoa.

Hii inwezekana kuwa ni ujio mpya wa msanii huyu kwa kutanguliza kiki na baadae kuachia nyimbo na video yake.

No comments

Powered by Blogger.