Header Ads


KESI YA ELIZABETH 'LULU' MICHAEL BADO MAMBO MAGUMU


 
Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili Lulu imesikilizwa tena leo kwa siku tatu katika mahakama kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
Muigizaji huyo ambaye jina lake halisi ni Elizabeth Lulu amekumbana na kikwazo baada ya shahidi wake muhimu,
Josephine Mushumbushi ambaye ni mke wa Dk Wilbroad Slaa kushindwa kufika sababu yupo nje ya nchi.Kutokana na hilo, Jaji Sam Rumanyika ameamuru polisi aliyechukua maelezo yake aende mahakamani Jumatano hii kesi itakapoendelea kutoa ushahidi badala ya Bi. Josephine.Lulu anayekabiliwa na kesi ya kusababisha kifo cha Steven Kanumba bila kukusudia, alikuwa ameongozana na wazazi wake mahakamani hapo.

No comments

Powered by Blogger.