Header Ads


Kitu ambacho Rosa Ree hawezi kuacha

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo Rose amesema ni vigumu kuacha kutumia lugha ya kingereza katika ngoma zake kwani muziki ni vile ambavyo mtu anataka kujielezea na si vinginevyo.

Rapper huyu ameendelea kwa kusema si kwake tu bali hata kwa wasanii wengine wanaweza kutumia lugha yoyote kufikisha kwa jamii kile ambacho wanakitaka kwa wakati huo.

“Huwezi kum-limit mtu kutumia lugha fulani katika muziki, kwani ni chombo cha kujielezea unavyohisi na kuelezea hisia zako kwa wakati ule, kwa hiyo kama wewe unahisi hisia zako zinakuambia imba kilugha fanya hivyo, kwa hiyo mimi hisia zangu ndio zinajielezea katika lugha ambazo natumia” Rosa Ree asema

“Ndio maana hata kwenye Up In The Air nilisema, watu walikuwa wanasema huyu demu anarap sana kingereza sana hajui Kiswahili nikawaambia siwezi Kiswahili nitakupa na kichaga kwa sababu kipaji cha Rosa Ree kinavuka mipaka is not about language” ameongeza.
Kwa sasa Rosa Ree anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Dow’ baada ya kufunika vilivyo na ngoma ‘Up In The Air’.

No comments

Powered by Blogger.