Header Ads


Niyonzima kufanya jambo mechi ya Simba na Yanga

Mwenyekiti maarufu zaidi wa klabu ya Simba kama utachukua wenyeviti wote, Hassan Dalali, hajapindisha mona baada ya kusema kiungo mpya wa Simba, Haruna Niyonzima ni fundi hasa na atafanya jambo siku ya mechi ya Yanga.

Dalali anaamini, Niyonzima atakuwa mhimili mkubwa wa Simba wakati ikiivaa Yanga, Jumamosi.

“Yanga hawako vizuri sana lakini hizi mechi za Yanga na Simba huwa hazina mwenyewe.

“Lakini Simba ina nafasi kubwa ya kucheza vizuri hasa katika upishi wa mipira. Kuna mtu kama Niyonzima pale, huyu ni fundi kwelikweli.

“Nasema kama Simba watafanya makosa nyuma wanaweza kushindwa, lakini lazima mpira wataucheza na wanachotakiwa ni kutumia nafasi kwa kuwa Niyonzima ambaye ni fundi kwelikweli na wenzake pale katikati watakuwa na msaada,” alisema.

No comments

Powered by Blogger.