Header Ads


Profesa Jay atupa jiwe gizani

Mbunge wa Jimbo la Mikumi Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay ametoa ujumbe unaoonekana kama ushauri kwa vyama vya siasa huku ukilenga matukio ya hivi karibuni ya wanasiasa kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine.

Katika Ukurasa wake wa mtandao wa Twitter Profesa Jay ameandika “Mkimaliza hiyo HOJA yenu Mfu ya UFISADI, leteni tuhuma za wote waliobaki huko na Muwatimue mapema msisubiri waondoke wenyewe... TUMEELEWANA”?

Ujumbe huu wa Profesa Jay umekuja ikiwa ni chini ya saa 24 toka Mbunge wa Singida Kaskazini kupitia CCM, Lazaro Nyalandu ajiuzulu Ubunge pamoja na nyadhifa zingine ndani ya chama ikiwemo kujivua uanachama.

Kwa upande mwingine ujumbe huo umechukuliwa kama jibu kwa Chama cha Mapinduzi ambacho kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole kilijibu suala la Nyalandu kuhama kwa hoja ya kuwa ni miongoni mwa wanachama wengi wasio waadilifu ambao wameamua kuondoka kabla ya Panga kuwafikia.

Hata hivyo Profesa Jay amegoma kufafanua undani wa ujumbe huo iwapo umelenga kupuuza hoja hiyo ya Ufisadi. Awali Profesa Jay aliandika ujumbe wa kumpongeza Nyalandu kwa uamzi wake na kumkaribisha Chadema. “Hongera sana my brother Lazaro Nyalandu kwa Ujasiri na kusimamia kile unachokiamini!! KARIBU SANA KIUMENI SPEAK YOUR MIND”, aliandika Profesa Jay.

No comments

Powered by Blogger.