Header Ads


Waziri Kalemani atoa maagizo mazito Tanesco, amfuta kazi mmoja

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewaagiza maafisa watatu wa TANESCO kuhakikisha umeme unarejea kote nchini hii leo la sivyo waandike barua ya kuacha kazi.

Dkt. Kalemani ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es salaam alipotembelea mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi One na Ubungo na kutaka maelezo ya kukosekana kwa umeme nchini tangu jana na baadhi ya maeneo leo hii.

Dkt. Kalemani amechukua maamuzi hayo baada ya kutoridhishwa na taarifa ya kukosekana kwa umeme kote nchini, huku akiagiza Meneja wa kituo cha kufua umeme cha Kidatu aondolewe mara moja na nafasi yake ichukuliwe na mtu mwingine mwenye weledi.

Maafisa waliopewa maelekezo hayo ni Mhandisi Isihaka Mosha-Meneja Udhibiti Mitambo, Mhandisi Bishaija Kahitwa-Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usafirishaji na Abdalla Ikwasa-Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uzalishaji.

No comments

Powered by Blogger.