Header Ads


Baada ya Lil Kim, sasa ni zamu ya Ashanti

Ikiwa ni siku chache toka mkali wa Hip Hop kwa wanawake Lil Kim kurejea katika game na ngoma yake ya ‘Took Us A Break’ naye mwanadada Ashanti ametanganza ujio wa ngoma yake mpya iitwayo ‘Say Less’.

Mrembo huyo ambaye alikuwa first lady wa Murder INC, amesha achia kava ya ngoma hiyo aliyomshirikisha rapper Ty Dolla $ign.

Mwezi Oktoba mwaka huu, mrembo huyo aliyewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Nelly alisika akisema neno ‘Say Less’ katika mahojiano aliofanya na Tmz kuhusiana na tuhuma za Ex wake Nelly kubaka.
Hata hivyo bado haijabainika kuwa ujio wa ngoma hiyo ni dongo kwa Nelly au ni jina la ngoma alikuwa akifanyia promo.

No comments

Powered by Blogger.