Header Ads


Beyonce apata shavu katika filamu ya animation ya The Lion King

Mambo yametimia. Hatimaye imethibitishwa kuwa Beyonce atakuwa mmoja ya waigizaji watakao ingiza sauti zao katika filamu ya animation ya ‘The Lion King’.

Mwezi Machi mwaka huu, Variety iliripoti kuwa mrembo huyo mwenye watoto watatu amekuwa chagua la kwanza kwa Disney ambao ni waandaaji wa filamu hiyo.
Kupitia mtandao wa Twitter, Disney wameweka picha za waigizaji ambao watashiriki katika filamu hiyo mmoja wapo ni Queen Bey ambaye ametumia jina la Nala.

Washiriki ambao watakuwepo katika The Lion King ni pamoja na Donald Glover (Simba), James Earl Jones (Mufasa), Chiwetel Ejiofor (Scar), Alfre Woodard (Sarabi), Seth Rogen (Pumbaa), Eric Andre (Azizi), John Oliver (Zazu), John Kani (Rafiki), and Billy Eichner (Timon).
Filamu hiyo inatarajiwa kutoka katika kipindi cha majira ya joto mwaka 2019.

No comments

Powered by Blogger.