Header Ads


Marco Asensio apiga bao la msimu La Liga

Nchini Hispania usiku wa jana mabingwa watetezi wa La Liga klabu ya Real Madrid ilifanikiwa kuchomoza na ushindi wa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya Las Palmas.

Madrid ikiwa nyumbani Bernabeu imeibuka na ushindi huo huku kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Marco Asensio akifanikiwa kufanga bao safi na linaloelezwa na wachambuzi wa soka barani Ulaya kuwa ni la msimu ndani ya ligi ya La Liga.
Asensio ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa ya Hispania amefunga bao hilo ndani ya mita 25 baada kupata mpira kutoka kwa kipa wa Las Palmas ambaye aliukoa kutoka eneo la lango lake.

Wafungaji wengine wa ushindi wa Madrid ni Casemiro dakika ya 41 na Isco akiifungia dakika ya 74 ya mchezo huo.
Real Madrid inashika nafasi ya tatu katika msimao wa ligi ya Hispania La Liga kwa kuwa na pointi 23 nafasi ya pili ikishikiliwa na Valencia wenye alama 27 na vinara ni timu ya Barcelona wenye jumla ya pointi 31.

No comments

Powered by Blogger.