Header Ads


Michezo Yanga SC, Simba SC na Azam FC kuzisaka pointi tatu muhimu wikiendi hii

Ligi Kuu soka Tanzania Bara inatarajia kuendelea tena hii leo kwa mchezo mmoja kuchezwa kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati mwenyeji Majimaji FC itashuka dimbani kuvaana na Stand United ya mkoani Shinyanga majira ya saa 10.00 jioni.

Mbali na Majimaji FC dhidi Stand United jumla ya michezo mitano inatarajiwa kupigwa wikiendi hii katika viwanja mbalimbali hapa nchini.
Singida United ikiwa katika Uwanja wake wa Namfua itaikaribisha Yanga SC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Kagera Sugar watakuwa wenyeji huko Bukoba katika dimba la Kaitaba watakapo wakaribisha Tanzania Prisons.
Njombe Mji wakiwa nyumbani katika dimba la Sabasaba Njombe watawakaribisha Mbao FC.
Azam FC itashuka katika Uwanja wa Azam Complex Jijini Dar es salaam kucheza na Ruvu Shooting.
Ndanda FC wakiwa mkoani Mtwara  watashuka katika Uwanja wa Nangwanda kucheza na Mtibwa Sugar.
Na hapo keshokutwa siku ya Jumapili ya Novemba 5 timu ya Lipuli FC ikiwa katika Uwanja wake wa nyumbani wa Samora mkoani Iringa itashuka dimbani kumenyana na Mwadui FC wakati Mbeya City itakuwa Sokoine Mbeya kuwakabili vinara wa ligi klabu ya Simba.

No comments

Powered by Blogger.