Header Ads


Nadal hakamatiki michuano ya Paris Masters

Mchezaji tenis namba moja katika viwango vya ubora duniani,Rafael Nadal anatarajia kumaliza mwaka huu huku akiwa anashikilia rekodi yake ya kuwa namba moja baada ya ushindi aliyoupata dhidi ya amefanikiwa Hyeon Chung kwenye duru la pili la michuano ya Paris Masters.

Mchezaji tenis namba moja katika viwango vya ubora duniani,Rafael Nadal
Rafael Nadal mwenye umri wa miaka 31, amemshinda mpinzani wake kwa jumla ya seti 7-5 6-3 ndani ya saa moja na dakika 48.

Mchezaji tenis,Rafael Nadal (kushoto) na Hyeon Chung (kulia)
Nadal ambaye ni raia wa Hispania mwanzo wa mwaka huu alikuwa namba tisa katika viwango vya ubora na kuanza kupanda kupitia ushindi wa michuano ya wazi ya Ufaransa (French Open) ile ya Marekani (US Open).
Kwa sasa anatarajia kucheza dhidi ya Pablo Cuevas raia wa Uruguay katika hatua ya 16 bora.

No comments

Powered by Blogger.