Header Ads


Wanawake 10 wenye nguvu ya ushawishi duniani mwaka 2017 watajwa

Jarida la Forbes Jumatano hii limetoa orodha mpya ya wanawake 100 wenye nguvu ya ushawishi zaidi duniani (100 Most Powerful Women ) mwaka 2017 kwenye Michezo, Sanaa, Teknolojia, Media na Siasa  wametajwa, ambapo orodha hiyo imeongozwa na Kansela wa Ujerumani Bi. Angela Merkel.

Wa pili kwenye orodha hiyo ni Waziri Mkuu wa Uingereza, Bi. Theresa May, wa tatu ni mke wa tajiri namba moja duniani Bill Gates, Bi. Belinda Gates, Tazama orodha kamili ya majina 100 HAPA.
Kwa upande wa majina ya wanawake waliofanya vizuri kwenye kipengele cha Burudani na Vyombo vya Habari (Media), Mwanamama Oprah Winfrey ameongoza orodha hiyo kwa mwaka 2017, huku akiwa nafasi ya 21 kwenye orodha nzima ya majina yote ya kwenye vipengele mchanganyiko.
Mwanamuziki Beyonce ameshika nafasi ya 5 kwenye orodha ya Wanawake wenye nguvu ya ushawishi zaidi duniani kwenye kipengele cha ‘Entertainment & Media’ huku akishika nafasi ya 50 kwenye orodha nzima ya wanawake wenye ushawishi zaidi duniani.
Aliyekuwa mgombea wa urais nchini Marekani mwaka 2016,  Bi. Hillary Clinton ameporomoka kutoka nafasi ya 63 mwaka jana 2016 hadi nafasi ya 65 mwaka huu hii ni baada ya kushindwa kwenye uchaguzi.

No comments

Powered by Blogger.