Header Ads


“Bado JPM anahitaji kuungwa mkono 2018”- Dr. Mwanjelwa

Naibu Waziri wa Kilimo Dr. Mary Mwanjelwa katika kusheherekea sikukuu ya Mwaka Mpya 2018 amewataka Watanzania nchini kote kuunga mkono kwa vitendo juhudi za uwajibikaji wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli.

Dr. Mwanjelwa ametoa wito huo January 1, 2018 wakati akitoa salamu kwenye ibada ya Siku ya Wazee iliyofanyika katika kanisa la Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus Healing Centre T. Ministry) lililopo Katika Jijini Mbeya.

 “Rais Magufuli na serikali anayoingoza anawathamini kwa kiasi kikubwa wazee kote nchini kwani kwa umri wao ni sehemu ya turufu muhimu kimawazo na busara katika utendaji” – Mwanjelwa

 “Serikali hii ya awamu ya tano inawakumbusha na kuwahamasisha wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kuinua haraka uchumi,” -Mwanjelwa

No comments

Powered by Blogger.