Header Ads


Neymar ashinda tuzo kwa kumbwaga Philippe Coutinho

Mchezaji ghali duniani kwa sasa wa PSG na timu ya taifa ya Brazil, Neymar da Silva Santos Júnior amefanikiwa kushinda tuzo ya Samba d’Or kwa mwaka 2017.

Neymar alifanikio kushinda kwa kupata kura asilimia 27.7 akifuatiwa na Philippe Coutinho wa Liverpool aliyepata asilimia 16.64.
Mchezaji huyo amefanikiwa kushinda tuzo hiyo kwa mara yake ya tatu sawa na mchezaji mwezake Thiago Silva wa PSG.
Tuzo ya Samba d’Or hupatiwa mchezaji wa Brazil anayecheza bara la Ulaya ambaye amefanya vizuri katika msimu husika. Tuzo hiyo ilianza kutolewa mwaka 2008.

No comments

Powered by Blogger.