Header Ads


Bill nass: Sipendi kuzushiwa kutoka kimapenzi na Wasanii


STAA ambaye kwa sasa anatamba na Wimbo wa Tag Ubavu, anayefahamika zaidi kwa jina la Billnass, amefunguka kuwa hakuna jambo ambalo linamkera kwa sasa kama kuzushiwa kwenye mitandao suala la mapenzi kutokana na ukaribu wake na wanamuziki wa kike.

Akichonga na Uplands fm kupiti Kipindi cha  XTRA FLAVA, Billnass alisema kwamba mwanzoni alizushiwa anatoka kimapenzi na Dayna Nyange na kwa sasa ishu ‘hot’ ni juu ya yeye kutoka kimapenzi na Rosa Ree, jambo ambalo halina ukweli wowote.

“Sipendi kuzushiwa kutoka kimapenzi na wasanii kwa sababu napata wakati mgumu kwenye uhusiano wangu wa kweli. Kiukweli skendo zinakuwa zinaniharibia maana hata yule niliyenaye wakati mwingine anafikiria ni kweli nina uhusiano na watu ninaotajwa nao, jambo ambalo linakuwa si la kweli,” alisema Billnass.

No comments

Powered by Blogger.