Header Ads


Huyu ndio msanii wa Afrika aliyetajwa kuwania tuzo za Kids’ Choice Awards 2018

Waandaaji wa tuzo za Kids’ Choice Awards 2018 wamemtaja msanii mmoja kutoka katika bara la Afrika ambaye atawania tuzo hizo zitakazotolewa Jumamosi ya Machi 24, mwaka huu.

Msanii huyo aliyetajwa kuwania tuzo hizo ni mshindi wa BET Awards 2016, kipengele cha Best International Act: Africa, Black Coffee kutoka Afrika Kusini ambaye ametajwa katika kipengele cha Favorite Global Music Star.

Wasanii wengine ambao wametajwa katika kipengele hicho ni BTS (Asia), Lorde (Australia/New Zealand), Maluma (South America), Taylor Swift (North America), The Vamps (UK), Zara Larsson (Europe).

Tuzo hio zitafanyika katika ukumbi wa The Forum, Californiana na vipengele takriban 17 vimetajwa wakati host atakuwa mchezaji wa mieleka wa WWE, John Cena.

No comments

Powered by Blogger.