Header Ads


John Bocco ahaidi makubwa Simba

BAADA ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) hivi karibuni kumtangaza mshambuliaji wa Simba, John Bocco kuwa mchezaji bora wa mwezi Januari, mwenyewe amesema kuwa kazi ndiyo kwanza imeanza.

TFF ilimtangaza Bocco kuwa mchezaji bora wa mwezi Januari baada ya kumbwaga mche­zaji mwenzake wa Simba, Mganda Emmanuel Okwi pamoja na Kiungo wa Mwadui FC, Awesu Awesu.

Akizungumza na Cham­pioni Jumatano kuhusi­ana na tuzo hiyo, Bocco alisema kuwa anashukuru kwa kuipata la­kini pia imemfanya aongeze bidii ili ku­hakikisha anaisaid­ia Simba kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

Alisema kuanzia sasa atahakiki­sha anapambana vilivyo uwanjani kila ataka­popewa nafasi ya kuitu­mikia Simba na atafanya hivyo bila ya kujalisha timu atakayokutana nayo.

“Nimefurahi kupata tuzo hiyo na imeniongezea nguvu ya kuhakikisha napambana vilivyo uwan­jani ili kuisaidia timu yangu kupata matokeo mazuri.

“Kwa hiyo kazi ndiyo kwanza imeanza, nitapambana kwelikweli na hata kama ni kufia uwanjani basi iwe hivyo,” alisema Bocco ambaye amejiunga na Simba msimu huu aki­tokea Azam FC na baada ya muda mchache akach­aguliwa kuwa nahodha wa timu hiyo.

No comments

Powered by Blogger.