Header Ads


Klabu ya ligi daraja la kwanza yaitoa Man City michuano ya FA.

Klabu  ya Wigan Athletic hapo jana ilizima ndoto za vinara wa ligi kuu ya Uingereza Manchester City kutwaa mataji mengi zaidi msimu huu baada ya kuitoa katika michuano ya FA kwa ushindi wa bao 1- 0.

Wigan Athletic walipata matokeo hayo baada ya klabu hiyo ya ligi ya daraja la kwanza nchini Uingereza kustahimili mikikimikiki  ya City katika harakati za kujiwekea ufalme wake wa kutwaa mataji mengi msimu huu.

Katika mchezo kulikuwa na vurugu za hapa na pale hasa baada ya shabiki wa Wigan kumvamia mshambuliaji wa Man City, Sergio Aguero katika mchezo huo uliyopigwa Uwanja wa  DW .

Hata hivyo katika mchezo huo uliyokuwa na mvutano mkubwa mchezaji wa Manchester City, Fabian Delph aliweza kupata kadi nyekundu na kutolewa dakika za kipindi cha kwanza.
   

No comments

Powered by Blogger.