Header Ads


Nataka walimu nao wapewe bunduki kulinda wanafunzi – Rais Trump

Rais wa Marekani, Donald Trump ameshauri walimu kupatiwa silaha ili kuwalinda wanafunzi na mashambulizi ya kutumia silaha za moto.

Rais Trump akihutubia wanafunzi na walimu White House.
Rais Trump amesema hayo jana Februari 21, 2018 wakati akihutubia wanafunzi na walimukatika hafla fupi ya saa moja iliyofanyika White House, Trump amesema huu ni muda muafaka kwa walimu kukabidhiwa silaha ili kuimarisha ulinzi mashuleni.
Najua watu wengi hawafahamu kuwa marubani wanamiliki bunduki za kujilinda na kuwalinda abiria pale linapotokea tatizo na ndio maana umeona matatizo yamepungua, kwa hiyo naona huu ni muada mwafaka walimu kukabidhiwa bunduki kwani Mwalimu mwenye bunduki anaweza kukabiliana na washambuliaji mara moja bila ya kusubiri askari polisi,“amesema Trump.
Kauli ya Trump inakuja ikiwa ni wiki moja imepita tangu wanafunzi 17 kuuawa kwa kushambuliwa kwa risasi na mwenzao mjini Florida.
Soma zaidi – Mwanafunzi auwa wenzake 17 kwa kuwapiga risasi
Hata hivyo, wazo hilo la Rais Trump liliungwa mkono na watu wote waliohudhuria kwenye hafla hiyo ambapo baadhi yao walimtaka abadilishe sera za umiliki wa silaha za moto.
Tazama hafla hiyo ilivyonoga wakati Trump akihutubia wanafunzi;

No comments

Powered by Blogger.