Header Ads


Picha: Jezi ya Man United iliyosainiwa na Mourinho yafika mezani kwa Conte

Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari mapema hii leo siku ya Alhamisi meneja wa Chelsea, Antonio Conte amekabidhiwa jezi ya Manchester United na Pranksters iliyosainiwa na kocha wa Man United, Jose Mourinh.

Watangazaji wa kipindi cha Italia 1 satirical show Le Iene , Alessandro Onnis na Stefano Corti walifanikiwa kukamilisha zoezi hilo baada ya jezi hiyo kusainiwa na Mourinho mwezi uliyopita huko The Lowry Hotel Manchester.

Mjumbe aliyefikisha jezi hiyo alimuonyesha Conte pia kipande cha video kutoka kwa Onnis na Corti kinachoelezea.
“Antonioooo, tume kutumia mjumbe kukuwakilishia jezi iliyosainiwa na rafiki yako mpya Joseee Mourinhoooo. Ametuambia kuwa anakupenda tazam alichokiandika hapo mbele ya  na kutupatia tukupe, rafiki yako , Jos amesema.” Ujumbe wa video kutoka kwa Onnis na Corti.

“Unaweza kutuahidi kuwa mchezo ujao utakao cheza dhidi yake mtakubaliana kuwa marafiki ?,  tuambie, Antonio urafiki wenu utadumu milele.”

Hata hivyo Conte ameonekana kusuasua kutoa majibu na kupokea jezi hiyo wakati wa mkutano huo mbele ya waandishi wa habari na kumtaka prankster kusubiri mpaka kumalizika kwa kikao hicho.

No comments

Powered by Blogger.